PROFESA JAY AMTABIRIA SUGU KUWA RAIS WA TANZANIA


Mbunge wa Mikumi (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa J’ amempongeza mbunge mwenzake wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kwa kuhitimisha mafunzo ya kisiasa na kusema sasa Sugu, anasubiri kuwa Rais wa Tanzania.


Profesa J ametoa utabiri huo leo Mei 11, 2018 bungeni kabla ya kuanza kuchangia kwa bajeti ya wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji ya 2018/19, ameanza kwa kusema;


“Natoa pongezi kubwa sana kwa pacha wangu aka Sugu kwa kuhitimu mafunzo huko ndani ambayo yameongeza ujasiri na CV yake ya kisiasa na natumaini sasa hivi hatakuwa rais wa Mbeya bali anakwenda katika mchakato wa kuwa Rais wa Tanzania huko mbeleni.”

Pongezi kama hizo, zimetolewa pia na mbunge wa viti maalum (Chadema), Devotha Minja ambaye amesema kilichompata Sugu ni harakati za ukombozi wa taifa hili.

Profesa J akichangia bajeti hiyo ya viwanda amesema mkoa wa Morogoro ulikuwa na viwanda vingi lakini vingi vimeshindwa kujiendesha na kushauri uchunguzi ufanyike, ili kuona wapi tumejikwaa.

Na Ibrahim Yamola, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527