Picha : SHIRIKA LA RAFIKI SDO LAFANYA SHEREHE KUWAAGA WAFANYAKAZI WAKE...SHUHUDIA HAPA


Jumatatu Aprili 30,2018 Shirika la Rafiki Social Development Organization – SDO la mkoani Shinyanga limefanya hafla ya kuwaaga wafanyakazi wake Shangwe Kimath na Kessy Sabato ambao wamepata kazii sehemu nyingine.

Shangwe Kimath alikuwa Afisa wa masuala ya Jinsia na mabadiliko tabia kupitia mradi wa SAUTI na sasa anakwenda katika shirika la kimataifa la Engenderhealth kutumikia nafasi hiyo kupitia mradi huo wa SAUTI unaotekelezwa katika mkoa wa Tabora na Singida.

Naye Kessy Sabato aliyekuwa Afisa Mradi wa Ulinzi wa mtoto,haki na utawala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga anakwenda wilayani Kahama kutumikia nafasi ya Afisa mtendaji kata ya Kinaga.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika usiku wa Aprili 30,2018 katika ofisi za Shirika hilo mjini Shinyanga,Mkurugenzi wa shirika la Rafiki SDO,Gelard Ng’ong’a alisema maafisa hao walikuwa wamelisaidia shirika kwa kiasi kikubwa kwani walikuwa wanafanya kazi kwa kujituma na uwezo wa hali ya juu.

“Tumeona ni vyema kuagana na ndugu zetu hawa kwa kula pamoja chakula cha usiku,kunywa na kufurahi pamoja,tumeishi nao vizuri,walikuwa wachapakazi wenye moyo wa kujitoa”,alieleza Ng’ong’a.

“Rafiki SDO inaongozwa na uwezo wa kufanya kazi,taratibu zetu za kazi ziko wazi hata mtu akiacha kazi kwetu pia kuna uwazi,tunafanya kazi kwa upendo,hatuna mambo ya ubaguzi wa rangi,ukabili,udini,ukanda,tunahitaji sisi ni mtu awe na uwezo wa kufanya kazi”,aliongeza.

Naye Meneja wa shirika la Kimataifa la Save the Children mkoa wa Shinyanga ,Benety Malima aliwataka maafisa hao kuendelea kufanya kazi kwa bidi huku wakimtumainia Mungu na kuwasihi kuendelea kuwa na moyo wa kukubali kukosolewa.

Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga,Anthony Gwandu aliwataka wafanyakazi wanaobakia katika shirika hilo kuiga kazi nzuri zilizokuwa zinafanywa na maafisa walioondoka katika shirika hilo.

Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wafanyakazi wa shirika la Rafiki na mashirika rafiki ya shirika hilo na wadau ilinogeshwa kwa muziki,chakula,vinywaji,zawadi na burudani mbalimbali.

Mwandishi wetu ,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio ametusogezea Video na picha 43 za matukio yaliyojiri…Tazama picha hapa chini 




Mkurugenzi wa shirika la Rafiki SDO,Gelard Ng’ong’a akizungumza wakati wa kuwaaga maafisa wawili wa shirika hilo Shangwe Kimath na Kessy Sabato usiku wa Aprili 30,2018 katika ofisi za shirika hilo mjini Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi wa shirika la Rafiki SDO,Gelard Ng’ong’a akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Meneja wa shirika la Save the Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima,kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga, Anthony Gwandu.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga,Anthony Gwandu akitoa neno wakati wa hafla hiyo.
Meneja wa shirika la Save the Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akitoa neno wakati wa hafla hiyo

Mfanyakazi katika mradi wa SAUTI,Dr. Deusdedith Mjungu akitoa neno wakati wa hafla hiyo
 Kessy Sabato aliyekuwa Afisa Mradi wa Ulinzi wa mtoto,haki na utawala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga anayekwenda wilayani Kahama kutumikia nafasi ya Afisa mtendaji kata ya Kinaga akiwaaga wafanyakazi wa shirika la Rafiki SDO.
Shangwe Kimath aliyekuwa Afisa wa masuala ya Jinsia na mabadiliko tabia kupitia mradi wa SAUTI na sasa anayekwenda katika shirika la kimataifa la Engenderhealth kutumikia nafasi hiyo kupitia mradi wa SAUTI unaotekelezwa katika mkoa wa Tabora na Singida akiwaaga wafanyakazi wa shirika la Rafiki SDO.
Mfanyakazi wa shirika la Rafiki SDO,Mwamini Haruna akitoa neno wakati wa hafla hiyo ambapo alisema waliishi vizuri na Shangwe Kimath na Kessy Sabato
Wafanyakazi wa shirika la Rafiki SDO wakicheza kwaito..
Burudani inaendelea wakati wa hafla hiyo
Mfanyakazi wa shirika la Rafiki SDO ,Neema akitoa neno la shukrani kwa wafanyakazi wanaoondoka katika shirika hilo
Wafanyakazi wa shirika la Rafiki SDO wakiwa katika eneo la tukio
Hafla inaendelea...
Wafanyakazi wa shirika la Rafiki SDO wakitafakari jambo
Meneja wa shirika la Save the Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akicheza muziki na wafanyakazi wa shirika la Rafiki SDO
Burudani ya muziki inaendelea
Shangwe Kimath akicheza na mmoja wa wafanyakazi wa shirika la Rafiki SDO
Mfanyakazi wa shirika la Rafiki SDO, Hadija Juma akipitisha shampen meza kuu kabla ya kuifungua wakati wa hafla hiyo
Hadija akijiandaa kufungua shampen
Hadija akifungua shampen
Wafanyakazi wa shirika la Rafiki SDO wakigonga cheers na meza kuu
Wafanyakazi wa Shirika la Rafiki SDO wakigonga cheers na waliokuwa wafanyakazi wa shirika hilo 
Ugongaji cheers unaendelea....
Cheers...
Shangwe Kimath akigonga cheers na Meneja wa shirika la Save the Children,Benety Malima (katikati) na Mkurugenzi wa shirika la Rafiki SDO, Gelard Ng'ong'a
Furaha eneo la tukio....
Kushoto ni MC Hasna Maige akitoa utaratibu wa kuchukua karatasi zenye maandishi ya aina mbalimbali ndani ya meza hapo mbele
Meneja wa shirika la Save the Children,Benety Malima akichukua karatasi
Wafanyakazi wa shirika Rafiki SDO wakifurahia jambo wakati wa zoezi la kuchukua karatasi zenye maandishi ya aina mbalimbali ambapo kila aliyechukua katarasi alikutana na maandishi yenye ujumbe mbalimbali
Hafla inaendelea...
Burudani ya muziki kama kawaida....
Keki maalumu wakati wa hafla ya kumuaga Shangwe Kimath na Kessy Sabato
Kushoto ni MC Hasna Maige akitoa utaratibu wa kukata keki 
Kulia ni Shangwe Kimath na Kessy Sabato wakikata keki..kushoto ni mfanyakazi wa shirika la Rafiki SDO Lydia Pius
Kessy Sabato akimlisha keki mkurugenzi wa shirika la Rafiki SDO,Gelard Ng'ong'a
Shangwe Kimath na Kessy Sabato wakilishana keki
Mfanyakazi wa Shirika la Rafiki SDO, Lydia Pius akitoa zawadi kwa Shangwe Kimath na Kessy Sabato
Mfanyakazi wa shirika la Rafiki Mwamini Haruna akitoa zawadi kwa Shangwe Kimath na Kessy Sabato
Kulia ni Mkurugenzi wa shirika la Rafiki SDO,Gelard Ng'ong'a akimpatia zawadi Shangwe Kimath
Kulia ni Mkurugenzi wa shirika la Rafiki SDO,Gelard Ng'ong'a akikumbatiana na Shangwe Kimath
Kulia ni Mkurugenzi wa shirika la Rafiki SDO,Gelard Ng'ong'a akimpatia zawadi Kessy Sabato

Wasaa wa chakula ukawadia...nyama choma ilikuwepo

Meneja wa shirika la Save the Children,Benety Malima akichukua chakula wakati wa hafla hiyo.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527