MBUNGE AISHAURI SERIKALI KUSITISHA ULAJI WA SAMAKI

Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba (CCM), amesema kuna haja ya serikali kusitisha ulaji wa samaki nchini kama uvuvi wa samaki hautakiwi.

Amesema pamoja na kwamba serikali inapiga vita kupitia operesheni sangara katika Ziwa Victoria, operesheni hiyo haiwezi kukubaliwa kwa sababu inaumiza wavuvi.

Kishimba ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya mwaka wa fedha wa 2018/19.

“Mji wa Mwanza umejengwa kupitia pamba na madini, na hao samaki wanaopigwa marufuku kuvuliwa nao wamechangia kwa sehemu kubwa ukuaji wa mji huo naiomba serikali iwagawie wavuvi vifaranga wa samaki ili zao la samaki liweze kuinufaisha serikali na wananchi kwa ujumla,” amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527