MAKONDA AWASIHI WASICHANA WA DAR WASIOLEWE NA WANAUME WAISHIO MABONDENI


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amewasihi wasichana katika mkoa wa Dar es salaam kutokubali kuolewa na wanaume ambao wanaishi katika maeneo ya bondeni ambayo ni hatarishi hasa katika kipindi cha mvua za masika.

Makonda amesema hayo leo Mei 17, 2018 alipofanya ziara katika eneo la Mbagala Kiburugwa na kuona badhi ya nyumba za wananchi ambazo zimeathirka kutokana na kujengwa katika maeneo hatarishi na kuwataka wakazi hao kahama mara moja.

“Nitoe rai kwa wasichana ambao hawajaolewa, usikubali kuolewa na mwanaume ambaye atakuonesha ana kiwanja bondeni, kataa huyo sio wa kukuoa sasahivi angalieni akina mama mnavyotaabika na nyumba zimebomoka hujui watoto wako unawalaza wapi” amesema Makonda.

Makonda ameongeza kuwa serikali haitaweza kutoa msaada wa chakula na malazi kila mara kwa wananchi ambao wanakumbwa na majanga yanayotokana na wao kuamua kukaa katika maeneo hatarishi kwa kujitakia.

Mkuu wa mkoa huyo amedai kuwa katika maeneo hayo ni ngumu kwa mwananchi kupata msaada wa dharura ikiwemo gari la wagonjwa au huduma ya zima moto

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527