JAMAA AITA POLISI ASAIDIWE KUTULIZA BALAA LA NGURUWE MTATA

Maafisa wa polisi hupokea simu zisizo za kawaida za watu wakiomba usaidizi, lakini kisa kimoja jimbo la Ohio kimewashangaza wengi. 

Polisi walipigiwa simu mapema Jumamosi na mwanamume aliyekuwa anahangaishwa na nguruwe.

Polisi walidhani pengine mwanamume huyo alikuwa anaota au alikuwa amelewa alipowaambia kwamba alikuwa anaandamwa na nguruwe akienda nyumbani.

"Tulifika kwa mwanamume huyo tuliyedhani alikuwa mlevi na kwamba alikuwa anaelekea nyumbani kutoka kwenye  saa 11:26 asubuhi," polisi hao wanasema kwenye Facebook.

Lakini walipofika walimpata mwanamume alikuwa hajalewa hata kidogo, lakini hakufurahia kabisa kufuatwa na nguruwe.

Alikuwa anafutwa na nguruwe lakini hakujua afanye nini, polisi wa kituo cha Ridgeville Kaskazini wamesema.

Mwisho wa ujumbe wa Facebook wa North Ridgeville Police Department

Polisi mmoja alifanikiwa kumkamata nguruwe huyo na kumuingiza kwenye gari la polisi na kumpiga picha.

Nguruwe huyo pia alipelekwa kwenye seli (chumba cha kuwafugia mbwa wa polisi) kabla ya kukabidhiwa kwa mmiliki wake Jumapili asubuhi.
Chanzo- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527