Serikali
imesema kuwa deni la jumla la taifa liliongezeka kwa Sh trilioni 3
katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Desemba hadi Machi mwaka huu.
Hayo
yamejiri mara baada ya Gazeti la Mwananchi kutoa taarifa zisizo sahihi
kuhusu deni hilo ambapo Serikali imetaka kupuuzwa kwa taarifa hiyo.
Aidha,
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Hassan Abbasi amelitaka gazeti la mwananchi kuomba radhi kwa umma kwa
siku mbili mfululizo kuanzia Jumapili kupitia ukurasa wa mbele wa gazeti
hilo na kwenye mitandao ya kijamii.
Hata
hivyo, Dkt Abbas ameongeza kuwa baada ya gazeti hilo kusisitiza kuwa
hawana nia mbaya, serikali imezingatia utetezi huo na inawapa nafasi ya
kujirekebisha zaidi.