WAZIKA WATU WAPEWA DILI DAR

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amezitaka halmashauri zote jijini kuajiri watumishi ambao watakuwa wanafanya kazi ya kuzika miili ya watu ambao watabainika kuwa hawana ndugu.

Meya Mwita ametoa kauli hiyo leo, kwenye kikao cha robo ya pili ya Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam, ambapo amewaeleza madiwani hao kuwa jukumu la kuzika marehemu wasiokuwa ndugu ni la jiji, kwakushirikiana na halmashauri hivyo wanapaswa kuwajibika katika hilo.

Amefafanua kuwa hadi sasa jiji limeshanunua gari pamoja na mahitaji mengine ya kuhifadhia miili hiyo pindi inatokea na kwamba changamoto iliyopo sasa ni watu ambao watashirikiana kutekeleza jukumu hilo.

“Mtakuabliana na mimi kwamba tulishakubaliana kwamba jambo hili lifanyike kwenye halmashauri zetu, lakini hadi sasa Kinondoni pekee ndio wametimiza agizo hili, sasa ninaagiza tena halmashauri nyingine za jiji hili kuajiri watu hao. Hivyo marehemu wanapokuwa wamekaa muda mrefu wanalazimika kuzikwa na jiji, natulikubali kuchangia usafiri,dawa na sanda,” amesema Meya Mwita.

Amefafanua kuwa watu wasiokuwa na ndugu wanapokufa, wanapokaa hospitalini zaidi ya siku 20,jiji linalazimika kuwazika hivyo wapo ambao wanazikwa kwenye halmashauri mbalimbali

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527