FISSOO : TANZANIA NI YA PILI BARANI AFRIKA KWA UZALISHAJI WA FILAMU


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo amewataka Watanzania kutumia vizuri fursa za masoko ya filamu kwa ajili ya kujiingizia kipato kwa sababu Tanzania ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa filamu barani Afrika ikitanguliwa na Nigeria.

Akizungumza Machi 23,2018 wakati wa uzinduzi wa Filamu ya "Laana ya Mke" katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema  ni lazima waigizaji watumie fursa zinazotengenezwa na Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo kwenye eneo la masoko ya filamu.

''Tunapozungumzia filamu Tanzania ni ya pili baada ya Nigeria, na ukizungumzia Tanzania pia Shinyanga ipo ndani yake kwa hiyo hii ni fursa kwenu ambapo bodi ya filamu na Wizara zinashirikiana kuhakikisha kazi za sanaa zinapata masoko'', alieleza Fissoo.

Aliweka wazi kuwa Bodi hiyo imekuwa ikifuatilia kila hatua ya wasanii hivyo kuwataka kuungana na kuepuka migogoro.

Filamu ya Laana ya Mke imeandaliwa na wasanii wa Bongo Movies Shinyanga ambao wamemshirikisha mwigizaji maarufu wa Filamu nchini Blandina Chagula 'Johari' ambaye kwao ni Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527