DIWANI WA KATA YA TURWA ZAKAYO CHACHA WANGWE NAYE AJIENGUA CHADEMA NA KUHAMIA CCM


Aliyekuwa Diwani wa kata ya Turwa Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara  Zakayo Chacha Wangwe kupitia chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA  akionyesha waandishi wa habari barua rasmi ya kujiuzulu Udiwani kwenye kata yake 
 na kuamua kuhamia Chama cha Mapinduzi CCM.
Barua iliyoandikwa na aliyekuwa Diwani wa kata ya Turwa Zakayo Chacha Wangwe.
Aliyekuwa Diwani wa kata ya Turwa kupitia CHADEMA Zakayo Chacha Wangwe akiongea na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Goldland Mjini Tarime leo Ijumaa Januari 5,2018.
Waandishi wa Habari wakiwa kazini. 
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Tarime Hamis Mkaruka Kura akiotoa Shukrani zake kwa Zakayo baada ya kupokelewa rasmi CCM.
Picha zote kwa hisani ya Cleo 24 News blog.

Diwani wa kata ya Turwa Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara kupitia chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na mjumbe wa kamati kuu ya Wilaya Chadema Zakayo Chacha Wangwe amebwaga manyanga na kukihama chama na kutimukia CCM.


Akizungumza leo Januari 5,2018 na waandishi wa habari katika ukumbi wa Goldland Hotel mjini Tarime Zakayo amesema kwa sasa haoni haja ya kuendelea kuwa kwenye chama ambacho hakuna dira na kuwashauri wanachama wengine wa vyama vya upinzani kujiunga CCM na kwamba amefikia uamuzi baada ya
kuridhishwa na utendaji kazi wa rais Magufuli.

Hata hivyo amewashukuru wananchi wake kumuunga mkono kipindi cha uongozi wake kwani umefanikiwa kupeleka maendeleo kwao ambayo ni tofauti na kipindi vingine vilivyopita huku akiwaomba kuendelea jumla ushirikiano katika kusukuma gurudumu mbele.

Na Waitara Meng’anyi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527