RAIS MAGUFULI AONGEZA BARAZA LA MAWAZIRI..ATEUA NAIBU WAZIRI MPYA WIZARA YA MADINI

Rais John Magufuli ameongeza baraza lake la mawaziri kwa kumteua Doto Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa kufuatia uteuzi huo Wizara ya Madini sasa itakuwa na waziri na naibu mawaziri wawili.

Biteko ambaye ni Mbunge wa Bukombe na alikuwa mwenyekiti wa kamati ya muda iliyochunguza madini ya Tanzanite.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi huo kwa lengo la kuongeza nguvu kutokana na uwingi wa majukumu katika Wizara ya Madini.

Biteko ataapishwa Jumatatu tarehe 08 Januari, 2018 saa 3:00 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527