MTOTO WA BABU SEYA ATOA KAULI FAMILIA YAO KUACHIWA HURU




Mtoto wa Mwanamuziki wa dansi Nguza Viking ‘Babu Seya’ Michael Nguza amesema anamshukuru Mungu baada ya Rais John Magufuli kutangaza familia yao ipo huru kuanzia leo Jumamosi Disemba 9,2017.


Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo, leo Jumamosi, Desemba 2017 akiwa mjini Dodoma wakati wa akihutubia maadhimisho miaka 56 ya sherehe za Uhuru wa Tanganyika.


Michael Nguza ambaye hivi sasa anajiita Nabii Michael baada ya kutoka jela amesema : “Namshukuru Mungu, Mungu ni mwaminifu. Siwezi kuongea mengi kwa sasa, nitatoa taarifa baadaye.


“Tunatarajia kufanya kikao cha familia ili kujadili suala hili na baadaye tutaulezea umma baada ya majadiliano haya familia naomba kuweni wavumilivu,” amesema Nabii Michael.


Na Bakari Kiango, Mwananchi 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527