BONANZA LA MBUNGE WA SEGEREA LAFANA

Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa amejumuika 
na wakazi wa jimbo lake katika bonanza lilijomuisha michezo mbalimbali.

Bonanza hilo lililofanyika katika uwanja wa Sigara uliopo Tabata 
lilikuwa ni hitimisho la mashindano ya Bonnah Cup 2017 ambapo fainali  ilikuwa ni kati ya Kimanga Bodaboda na Sigara FC huku timu ya Bodaboda  ikiibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4.

Mshindi wa fainali alijishindia shilingi  milioni moja taslimu pamoja na pikipiki wakati mshindi wa pili akipata  shilingi laki tano na mshindi wa tatu akiondoka na shilingi laki tatu.

Akizungumza baada ya fainali  Mheshimiwa Bonnah Kaluwa amesema mashindano hayo yatakuwa endelevu kila  mwisho wa mwaka ili kuinua michezo jimboni hapo na kusema mshindi wa  mwaka huu atapata nafasi ya kwenda Dodoma kushindana na timu ya wabunge.
Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya Bodaboda Kimanga kabla ya mchezo wa fainali
Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa katika picha ya pamoja na EFM jogging club
Mheshimiwa Bonnah Kaluwa akionyesha umahiri wa kupiga danadana akitazamwa na wachezaji wa zamani wa Taifa Stars
Mshambuliaji wa timu ya Sigara FC akijaribu kuwatoka mabeki wa Bodaboda
Mamia ya mashabiki wakifuatilia mchezo
Wachezaji wa Bodaboda Kimanga wakifurahia kombe lao
Mheshimiwa Bonnah Kaluwa akiungana na mashabiki kucheza singeli 
Mkali wa muziki wa Singeli Msaga Sumu akiwaburudisha mashabiki waliojitokeza kwa wingi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527