AHADI 10 ZA MO DEWJI BAADA YA KUSHINDA ZABUNI YA KUWA MWEZESHAJI WA SIMBA

Bilionea Mohammed Dewji ameipokea kwa mikono miwili ishu yake ya ushindi kuwa mwekezaji mpya Simba na ametoa ahadi zake 10 kuhakikisha zinafanyika kuleta mabadiliko makubwa.

Mo Dewji ameshinda zabuni ya kuwa mwekezaji wa Simba kwa dau la Sh bilioni 20 alizoweka ‘mezani’ na hakukuwa na mtu yoyote aliyejitokeza kushindana naye kama ilivyokuwa ikielezwa awali.

MOJA:
Kambi ya Simba itajengwa upya kabisa na itakuwa ni hosteli ya kisasa yenye vyumba hadi 35. 30 vitakuwa kwa ajili ya wachezaji na vitano kwa ajili ya benchi la ufundi.
 
MBILI:
Simba sasa itafaidika kwa kuwa na gym yake ya kisasa, bwawa kubwa la kuogelea kwa ajili ya mazoezi na sehemu ya kupumzika kwa wachezaji.
 
TATU:
Wachezaji, makocha na viongozi watakuwa na mgahawa wao wa kisasa kabisa.
 
NNE:
Mo Dewji anaamini timu lazima iwe na viwanja vya mazoezi. Hivyo ataanza na viwanja viwili, kimoja nyasi asilia na kingine nyasi bandia.
 
TANO:
Mo Dewji ameahidi kuwekeza katika soka la vijana akianza na wale wenye umri wa chini ya miaka 14, 16 na 18 na lengo ni kuwakuza.
 
SITA:
Mo Dewji amesema atasimamia wachezaji kuitambua thamani ya Simba kwa kujituma hasa.

SABA:
Simba itaanza kufanya mambo kimataifa kwa kuitangaza na kuikuza brand ikiwa ni pamoja na kutengeneza vifaa mbalimbali kama fulana, kofia, vishika ufunguo na kadhalika.

NANE:
Ameahidi kutenga kitita cha  Sh milioni 500 ambazo zitatumiwa na benchi la ufundi katika mipango yao kama kambi na kadhalika pia Sh bilioni moja kwa ajili ya usajili.

TISA:
Kushindana na timu kubwa Afrika na sio Tanzania pekee.

KUMI:
Kurejesha Simba katika historia ya kimataifa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527