YUSUPH MANJI ANYANG'ANYWA SHAMBA NA SERIKALI

Serikali imelifuta shamba la mfanyabiashara Yusuf Manji, lenye ukubwa wa eka 714.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema leo Jumatano kuwa, shamba hilo litapangiwa matumizi mengine.


Lukuvi amesema shamba lingine la kampuni ya Amadori lenye ukubwa wa eka 5,400 pia limefutwa.


Waziri amesema mashamba hayo sasa yako mikononi mwa Serikali na yatapangiwa matumizi mengine.


Lukuvi amewaonya wananchi wasivamie maeneo hayo kwa kuwa watakaokamatwa watashitakiwa.


"Muyaache maeneo hayo kama yalivyo mkijenga tutakuja kuvunja," amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527