TCRA YAWAONYA WAMILIKI WA MITANDAO YA KIJAMII

Wamiliki wa mitandao ya kijamii wameaswa kuchuja habari zao ambazo wamekuwa wakizipata na kuzisambaza kwa jamii kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa Redio ama televisheni za Mitandaoni.

Hayo ameyasema leo Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui , Valerie Msoka wakati alipokutana na baadhi ya wamiliki wa mitandao ya Kijamii pamoja na waandishi wa habari.


Valerie amesema kuwa upashanaji wa habari lazima kuangalia na usalama wa nchi pamoja kuacha uchochezi ambao unachonganisha jamii au mamlaka.


Amesema kuwa takribani miaka mitano kulikuwa hakuna fursa za kupata matangazo ya televisheni kupitia mitandao ya kijamii, lakini sasa imeenea kwa watanzania wengi na inaendelea kuongezeka kadri ya teknolojia inavyokuwa, hivyo kunahitajika kuwepo umuhimu wa kusimamia huduma ya mitandao hiyo ili iweze kuleta tija kwenye taifa na si vinginevyo.


Valerie amesema kuwa TCRA kupitia kamati ya maudhui inatambua na kuthamini kuwepo kwa fursa ya upashanaji wa habari na serikali iliamua kuruhusu huduma hiyo wakati miongozo na taratibu stahiki zikiendelea kutayarishwa.


Amesema vyombo vya habari katika mitandao ya kijamii vya Radio, Televisheni na bado teknolojia inaendelea kukua na haviwezi kuzuia kutokana na mfumo wa upashanaji wa habari. 


Mwenyekiti huyo anasema habari zingine hazina tija kwa jamii na zingine zinaleta uchochezi ndani ya jamii na wakati mwingine kuingilia faragha za watu ambazo hazitakiwa kufikia jamii kama sehemu ya habari.


Amesema wadau wa mitandao ya kijami na watumiaji wa mitandao hiyo wanahakikisha wanahabarisha kwa kuzingatia habari zinazojenga umoja wa kitaifa, mshikamano na ushirikiano baina ya watanzania bila kujenga hofu, kuchochea chuki na uhasama baina ya watanzania. 


Aidha amesema habari za matusi katika mitandao ya kijamii hayavumiliki ,kwani zinakiuka misingi ya uandishi na uhuru na wajibu wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527