Picha: SHUWASA YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA HOTELI,NYUMBA ZA KULALA WAGENI SHINYANGA MJINI


Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Injinia Silvester Mahole akizungumza katika warsha ya kundi la wafanyabiashara wa hoteli na nyumba za kulala wageni mjini Shinyanga leo Ijumaa Agosti 4,2017. Kushoto ni mwenyekiti wa warsha hiyo Willium Shayo ambaye ni Mkurugenzi wa Evergreen Guest House ,kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog


*******

Ijumaa Agosti 04,2017 Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) imekutana na kundi la wafanyabiashara wa Hoteli na Nyumba za Kulala Wageni (Guest House and Logde) mjini Shinyanga kwa lengo la kuwapa uelewa jinsi Mamlaka inavyojiendesha sambamba na kupata maoni kutoka kwa wadau hao na kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha huduma.

Akizungumza katika kikao hicho,Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla alisema utoaji wa huduma kwa wananchi una changamoto nyingi ambazo njia pekee ya kuzitatua ni kushirikisha wadau wote.

“Mamlaka imekuwa ikitoa elimu kwa wadau kuhusu namna mamlaka inavyojiendesha na kadri wadau wanavyoelewa kuhusu haki na wajibu wao ndivyo wanavyoweza kushiriki kikamilifu kutatua changamoto zinazojitokeza hivyo kuleta mshikamano zaidi baina ya mamlaka na wadau wake”,alisema Mwenyekiti.

Wakichangia hoja katika warsha hiyo,wafanyabiashara hao walisema kero kubwa waliyohitaji ifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo ni kukosekana kwa Mfumo wa Majitaka hali inayosababisha watumie gharama kubwa kwa ajili ya huduma ya kuondoa majitaka katika maeneo yao ya biashara.

Meneja wa Karena Hotel Richard Luhende alisema kukosekana kwa mfumo wa majitaka kunawasababishia hasara akitolea mfano wa hoteli hiyo kuita magari ya majitaka walau mara tatu kwa wiki.

Naye Meneja wa Kisindi Lodge Agnes Nyamwihula aliomba wafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa uadilifu ikiwa ni pamoja na kusoma mita zilizowekwa nje ya nyumba kwani baadhi ya mita huwa hazisomwi matokeo yake Ankara ya maji inakuwa kubwa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Injinia Silvester Mahole alisema mamlaka hiyo ipo katika mkakati wa kuwa na mfumo wa majitaka mjini Shinyanga ingawa gharama za kuendeshea mradi wa majitaka ni kubwa.

“Tayari tumeshapata eneo la kufanyia mradi huu,tunafanya jitihada za kutafuta wafadhili,tatizo ni kwamba wafadhili wengi wanaogopa kuwekeza katika mradi wa maji taka kutoka na gharama zake kuwa kubwa zaidi ya mradi wa maji safi”,aliongeza Injinia Mahole.

Katika hatua nyingine alitumia fursa hiyo kuwahamisha wateja wa mamlaka hiyo kutumia njia za kisasa kulipia Ankara zao kama vile kulipa kwa njia ya M-PESA,TIGO PESA au benki ya NMB au Benki ya CRDB.

“Tunawashauri wateja wetu kubadilika kulingana na maendeleo ya sayansi na teknolojia,tumeboresha huduma zetu kwa kiwango cha juu sana,mbali na kulipa bill kwa njia ya simu,hivi sasa unaweza kulipa kwa njia ya benki”,alieleza Injinia Mahole.

Injinia Mahole alizitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na gharama kubwa za uendeshaji,uhaba wa nyenzo za kufanyia kazi,bomba za spea na presha kubwa ya maji kutoka Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria hali inayosababisha kupasuka kwa mabomba.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla akifungua warsha ya kundi la wafanyabiashara wa Hoteli na Nyumba za Kulala Wageni (Guest House and Logde) iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) leo Ijumaa Agosti 4,2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Injinia Silvester Mahole akizungumza katika warsha ya kundi la wafanyabiashara wa hoteli na nyumba za kulala wageni mjini Shinyanga.
Injinia Mahole akizungumza katika warsha hiyo.Kushoto ni mwenyekiti wa warsha hiyo William ShayoWillium Shayo ambaye ni Mkurugenzi wa Evergreen Guest House,kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla.
Mwenyekiti wa warsha hiyo William ShayoWillium Shayo ambaye ni Mkurugenzi wa Evergreen Guest House akizungumza wakati wa warsha hiyo. 
Shayo akizungumza ukumbini.
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Injinia Silvester Mahole akielezea kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakisikiliza kwa umakini mada iliyokuwa inaendelea.
Warsha inaendelea.
Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard akielezea kuhusu Haki na Wajibu wa mteja wa SHUWASA ambapo aliwasisitiza wananchi kuwafichua watu wanaohujumu miundo mbinu ya mamlaka hiyo na kuwaasa kulipa ankara kwa wakati na kuepuka kutumia mafundi wa mitaani.
Sehemu ya mada ya Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard 
Meneja Biashara wa SHUWASA, Reuben Mwandumbya akielezea kuhusu sheria inayohusu wizi wa maji.
Meneja wa Karena Hotel Richard Luhende akichangia hoja ukumbini.
Meneja Ufundi wa SHUWASA, Geofrey Hilly akizungumza ukumbini.
Meneja wa Kisindi Lodge Agnes Nyamwihula akichangia hoja katika warsha hiyo.
Meneja wa Katemi Hotel,Lameck Ntule akichangia hoja ukumbini.
Warsha inaendelea.
Afisa Rasilimaliwatu na Utawala wa SHUWASA,Kambira Mtebe ambaye alikuwa MC katika warsha hiyo akikisisitiza jambo ukumbini.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa ukumbini.

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527