MGEJA AMSHANGAA KINANA KUKIRI MADUDU YA CCM HADHARANI...AMTAKA AACHE KUWAHADAA WATANZANIA

Mwenyekiti wa Tanzania Mzalendo Foundation Khamis Mgeja

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana katika harakati mbalimbali za kujenga chama mkoani Shinyanga kabla Mgeja kutimkia Chadema mwaka 2015. (Picha kutoka Maktaba ya Malunde1 blog) 

******
MWENYEKITI wa Tanzania Mzalendo Foundation (Taasisi inayoshughulikia utawala bora na haki za binadamu) Khamis Mgeja amemtaka Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahaman Kinana aache kuwahadaa na kuwafanya watanzania kuwa watoto kwa kukiri hadharani madudu yaliyofanywa na serikali za awamu zilizopita kuwa yanarekebishwa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli.

Mgeja ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga,kisha kutimkia Chadema,alisema hayo Agosti 4,2017 wakati akiongea na waandishi wa habari mkoani Kigoma akiwa njiani kuelekea Dar es Salaam.

Alisema Kinana alitamka maneno hayo juzi katika ziara ya rais Dk. John Magufuli mkoani Tanga alipopewa nafasi ya kuzungumza na wananchi eneo la Mkanyageni wilaya ya Muheza.

Mgeja alinukuu maneno ya Kinana kuwa …"Jitihada
zinzofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kurekebisha makosa ni sahihi na hakuna tatizo lolote kufanya hivi kutokana na ukweli kuwa awamu ya seriakali zote zilizopita na ya sasa ni za CCM na kama kuna makosa yaliyofanywa na awamu zilizopita hakuna shida kwa sababu hata anayerekebisha ni wa CCM lakini kama alieharibu ni wa CCM mimi sioni
tatizo hivyo tuache kualalamika",mwisho wa kumnukuu.

Mgeja alisema amesikitishwa na kauli ya Kinana.

"Kinana ni  kaka yangu ninayemheshimu sana lakini kauli zake zimenisikitisha mimi nawatanzania kwani ni nyepesi mno hasa katika masuala mazito ambayo taifa limeathirika na uongozi mbovu wa serikalizilizopita ikiwemo ufisadi,wizi,uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya madaraka",alisema Mgeja.

"Kinana atambue kuwa leo hii taifa linanuka umaskini wa kutupwa kwa sababu ya mikataba mibovu ya rasilimali za nchi zilizofanywa kwa maksudi na watawala waliokabidhiwa dhamana na wananchi ikiwemo na CCM na kupelekea wananchi kushindwa kunufaika na rasilimali zao walizotunukiwa na Mungu",alisema.

"Tulitegemea Kinana atoe tamko kama chama aelekeze serikali ya awamu ya tano na watawala wote walioitumbukiza nchi katika
lindi la umaskini wafikishwe mahakamani haraka iwezekanavyo  kama wanavyofanya nchini Malawi kwa rais mstaafu Joyce Banda kwa ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka",alieleza Mgeja.

"Kauli alizotoa Kinana sijui anamfurahisha nani kwani makosa hayo yaliyofanywa na serikiali zilizopita siyo ya kurekebishwa kwa hiyo hayarekebishiki zinahitaji hatua kali za kisheria watanzania wanataka waone kuliko kulindana kama kuna kinga ziondolewe kwa misingi ya katiba na sheria",aliongeza.

Mgeja  alieleza kuwa alitegemea Kinana kama katibu mkuu wa CCM taifa angewaomba radhi watanzania kwa yale yaliyofanywa ya ufisadi,wizi na matumizi mabaya ya madaraka kwa serikali zilizopita kama chama chake cha CCM ndicho kilichopewa dhamana kuongoza taifa hili hivyo ubadhirifu huo kama
chama lazima kibebe lawama na kuwajikiba kwa wananchi.

Alisema alimkumbusha Kinana  kwamba atambue kuwa watazania wa leo siyo wakudanganyika kwani wanajitambua hivyo hakuna wa kuwadanganya wala wa kuwahadaa.

Na Hastin Liumba - Kigoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527