WASICHANA WANG'ARA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2017



Matokeo ya kidato cha sita nchini yalitolewa leo Jumamosi, Julai 15, 2017 yameonyesha kuwa wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo kati ya wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni ni 27,577 (sawa na asilimia 97.21).


Jumla ya watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu.


Kwa upande wa watahiniwa wavulana, waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34) kati ya 46,385.


Taarifa iliyotolea inaonyesha kuwa watahiniwa 58,556 (asilimia 93.72) walipata daraja la kwanza hadi la tatu. Kati ya hao, wasichana ni 22, 909 na wavulana ni 35,647.


“Mchanganuo wa ufaulu katika madaraja unaonyesha kuwa watahiniwa walipata daraja la 1-11 umepanda kwa asilimia 0.59 kutoka asilimia 93.13 mwaka 2016 hadi 93.72 mwaka huu,” imesema taarifa hiyo na kuongeza;


“Pia, ufaulu katika madaraja kwa upande wa wasichana umepanda ikilinganishwa na wavulana. Ubora wa ufaulu kwa wasichana ni asilimia 94.07 ikilinganishwa na asilimia 93.49 ya wavulana.”


Ufaulu wa masomo
Kadhalika taarifa hiyo imeonyesha kuwa ufaulu kwa watanikiwa wa shule kwa upande wa masomo, ya Sayansi, Biashara, Lugha na Sanaa, haukuonyesha tofauti kubwa ukilinganisha na mwaka jana.


Hata hivyo, ufaulu katika somo la General Studies umeshuka kwa asilimia 7.54 kutoka asilimia 71. 24 hadi 63.70.

Angalia hapa chini Matokeo hayo


 
Poleni kwa ususmbufu mliopata siku ya leo wa kuhangaika kutafuta Link sahihi inayoweza kukuonesha matokeo ya kidato cha sita 2017 yaliyotangazwa leo .Hii hapa chini ni link sahihi inayofungua matokeo hayo bila matatizo.Bonyeza link hii hapa chini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527