JULIO ABADILI MAWAZO...SASA KUREJEA KUFUNDISHA SOKA TANZANIA BAADA YA KUSUSA

Jamhuri Kihwelu " Julio ",kocha mwenye maneno mengi asiyeishiwa na vituko,ametamka kurejea katika soka la Tanzania,akiwa katika nafasi yake ya Ualimu wa soka,ambayo aliisusa kwa madai aliyotoa kuwa kandanda la Tanzania,limetawaliwa na ubabaishaji.


Kocha huyo wa zamani wa Simba,Coastal Union, Mwadui Fc,amesema anamipango wa Kurejea katika soka kamaKocha Licha ya msimu wa Uliopita Akiwa kama Kocha wa Mwadui kutangaza kuachana na Ukocha kutokana na mizengwe Iliyopo katika Soka.

Julio amesema anaamini wale waliokuwa wakileta Mizengwe katika Soka wanaelekea kutoka katika soka Hilo na Tayari Kuna Vilabu Ligi Kuu na Ligi daraja la Kwanza vimeshaonyesha nia ya Kumwitaji

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527