KAULI YA JERRY MURO BAADA YA TFF KUMFUNGIA HAJI MANARA KUTOJIHUSISHA NA MAMBO YA SOKA MWAKA MMOJA

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemfungia Haji Manara (Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba) kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja na pia anatakiwa kulipa faini ya Shilingi  Milioni tisa.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Jerome Msemwa amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya Manara kukutwa na makosa matatu dhidi ya TFF ambao ni walalamikaji.

Makosa hayo ya Manara dhidi ya mlalamikaji TFF ni kuituhumu na kuidhalilisha TFF, kueneza chuki za ukabila na la tatu kuingilia utendaji wa shirikisho hilo.
 
Siku chache zilizopita  Manara aliituhumu TFF kufanya njama za waziwazi ili kuwabeba wapinzani wao Yanga kwenye Ligi Kuu.

Manara pia aliwatuhumu viongozi wakuu wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu wake, Selestine Mwesigwa ni wahaya na viongozi wa zamani wa Yanga, ambao wanataka kuipendelea Kagera Sugar.


Muda mfupi  baada ya shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kamati ya nidhamu ya TFF kutangaza kumfungia mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara kwa utovu wa nidhamu na kukutwa na makosa matatu.

Afisa habari wa zamani wa Yanga ambaye nae alifungiwa mwaka mmoja Jerry Muro ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika“Mtuache sasa tupumzike, tuliyofanya kwa taifa hilo haswa kwenye mpira nadhani yametosha, Waswahiba karibu kijiweni @hajismanara“

Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka pamoja na faini ya Tsh Milioni 9.

Kamati ya nidhamu ya TFF imetoa adhabu hiyo licha ya Haji Manara kushindwa kufika kwa madai ya kupata dharura lakini anayo nafasi ya kukata rufaa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527