MTOTO WA CHEKECHEA ABAKWA 'ANAJISIWA' SHULENI



WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekemea vikali tukio la kunajisiwa kwa binti wa miaka saba (jina limehifadhiwa) mkazi wa Kata ya Kitanzini, mwanafuzi wa darasa la awali katika Shule ya Sun Academy iliyoko Kata ya Kwakilosa katika Manispaa ya Iringa.

Taarifa ya Wizara iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Erasto Ching’oro imesema Serikali kupitia wizara hiyo imesikitishwa na taarifa za awali kuwa, mtoto huyo alinajisiwa katika mazingira ya shule mahali panapotarajiwa kuwa salama kwa watoto kuishi.

“Serikali imekuwa ikisisitiza walezi wa watoto kuhakikisha wanalinda watoto dhidi ya vitendo vyote vya ubakaji kwani vimekuwa vikitaarifiwa kuwahusisha watu wa karibu wanaomzunguka mtoto katika familia, shuleni na jamii.”

“Wizara inapongeza vyombo vya habari vyote vinavyoibua matukio ya ukatili, kwa kufanya hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambao utekelezaji wake unahusisha wadau wote nchini,” ilieleza taarifa hiyo.

Ching’oro katika taarifa hiyo amesema wizara inaamini Polisi kwa kutumia weledi wao watashirikiana na wananchi, walezi, walimu na marafiki wa mtoto, kuwasaka na kuwabaini.
Chanzo-Habarileo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527