Rais Magufuli : Wapinzani Walisusia Vikao Vya Bunge Kwa Sababu Wanajua na Wao ni Part ya Mafisadi..Nitawanyoosha


 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana July 29 2016 alianza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma ambapo alizungumza na wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.



Akizungumza na wananchi wa Manyoni mkoani Singida Rais Magufuli alizungumzia kuhusu wabunge wa upinzani kususia bunge kwa kujiziba midomo na makaratasi


Alisema wabunge hao wa upinzani waliamua kususia bunge kwa sababu kilichokuwa kikijadiliwa ndani ya bunge ni mahakama ya mafisadi na wao (wapinzani) ni sehemu ya mafisadi .


"Hawakuingia kwenye bunge kwa sababu walijua ni part ya hao mafisadi, nataka nieleze hawatapenya mbele ya serikali yangu, mafisadi lazima wanyooke" Alisema Rais Magufuli.
 Msikilize hapa akiongea

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527