Maajabu!! MZEE AZIKWA AKIWA AMEKAA NDANI YA JENEZA

Jeneza la Kiti
Kuna taarifa ambazo kama ukibahatika zikakufikia, zinaweza kukuacha kinywa wazi ama kukushtua kwa namna fulani.

Habari kutoka 254 Kenya ni ile inahusiana na mazishi ya aina yake ambapo familia moja imefanya mazishi ya mzee wao aliyekuwa akifahamika kwa jina la Adriano Aluchio anayetajwa kuwa mzee wa kuheshimika kwenye jamii hiyo akiwa amekaa ndani ya jeneza lilichongwa kwa namna ya kipekee tofauti na ilivyozoeleka.
Baadhi ya watu waliohojiwa kuhusiana na tukio hilo wamesema ni utamaduni wa jamii ya kabila la Lughia kufanya mazishi ya namna hiyo kwa mzee aliyeheshimika, kwa imani kuwa amefariki lakini anaendelea kuwalinda watoto wake pamoja na jamii yake.
Moja ya wazee katika jamii hiyo amenukuliwa akisema, “Mazishi kama hayo ya kumkalisha marehemu yalianza tangu zamani sana wakati wa mfalme Nabongo Mumia, na sisi tulitokea katika jamii hiyo, tukimzika amelala hatoridhika… Ataonekana akitembea huku juu….”
Baada ya mazishi hayo ya kipekee, walichukuliwa ng’ombe dume wawili na kupiganishwa juu ya kaburi kama njia ya kufukuza mapepo wachafu, huku wanakijiji wakipongeza kitendo cha mzee huyo kupewa mazishi ya hadhi.
Jamii ya Waidakho katika kabila la Walughia wanoishi katika Kaunti ya Kakamega wanajulikana sana kwa mchezo wao unaowavutia watalii eneo hilo la kuwapiganisha Fahali na kuku Jogoo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527