Ni muda mfupi tu toka Uganda ipitishe
sharia ya kupinga ushoga, imeripotiwa mtu mmoja aliyetuhumiwa kuwa shoga
alichomwa moto mpaka kufa nchini humo.
CNN
imeripoti tukio hilo ambalo jina la mtu (KULIA PICHANI) huyo halikuweza
kujulikana.
Picha ilionesha jinsi mtu huyo anavyochomwa moto huku akiwa
pembeni mwa reli huku watoto wakishuhudia tukio hilo.
Sheria hiyo iliyopitishwa hivi karibuni, inahusisha pamoja na kufungwa
maisha kwa mtu yoyote atakayejihusisha na shughuli zozote za ushoga
pamoja na kuambukiza ukimwi, matendo ya ngono na watoto pamoja na watu
wenye ulemavu, udhalilishaji ikiwa ni pamoja na ubakaji.
Sharia
hiyo iliyozaliwa mwaka 2009, na kupewa jina “Kill The Gays” ikimaanisha
“Ua Mashoga” ambayo ilisisitiza hukumu ya kifo kwa matendo fulani ya
ushoga, lakini ilirudishwa kabatini kutokana na kelele nyingi
zilizopigwa na mataifa mbalimbali.
Katika sheria hii mpya, mtu yeyote atakaye fungisha ndoa ya jinsia moja
atahukumiwa kifungo cha mpaka miaka 7. Atakayeshindwa kutoa taarifa ya
ushoga polisi pia ni muharifu.
Madaktari watakao watibu mashoga, watakaopangisha mashoga kwenye nyumba
zao na wale wataka shukiwa kuwa mashoga, wasagaji, waliobadilisha jinsia
na mabasha watafungwa miaka 5.
Mtu yeyote atakayetoa msaidia kwa shoga atakuwa anavunja sharia, ambapo atachukuliwa hatua.
Watu wengi wanaamini kuwa sharia hii ni muhimu ili kupinga tabia na
tamaduni za nchi za magharibi.
“ hii sharia ni muhimu kwa nchi hii ili
kulinda tamaduni za Mwafrika” alisema David Bahati ambaye ni mbunge
ambaye aliuwakilisha muswada huo bungeni.
Bahati pia ni mmoja kati ya kundi linalotuma fedha katika nchi za Afrika kuunga mkono wanaopinga shughuli zote za ushoga.
CREDIT - USWAZI24
Post a Comment